|
Yohana
alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo
ondoleo la dhambi. Marko 1:4
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye. Luka 7:29-30 |
|
Basi
tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi
kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo
hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Warumi 6:4
Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. Tito 3:5 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Mathayo 3:11 |