|
Ni neno
la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. 1Timotheo
3:1
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Matendo ya Mitume 20:28 |
|
Nawasihi
wazee walio kwenu, mimi niliye
mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa
utukufu utakaofunuliwa baadaye; lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu,
na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu
atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama
wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa
lile kundi. 1Petro 5:1-3
|